Habari

Tina Tunner aamua kuwa tofauti, avaa gauni la kijani katika harusi yake

Mwimbaji mkongwe Anna Mae Bullock maarufu kwa jina lake la jukwaani Tina Tunner mwenye miaka 73, weekend iliyopita amefunga ndoa na Erwin Bach iliyofuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika huko Switzerland.

Tia Tunner wedding

Tumezoea kuona mwanamke akivaa vazi jeupe katika tukio la kufunga ndoa kitu ambacho Mrs Erwin aliamua kujitofautisha na wengine na kuvaa gauni la kijani katika ndoa hiyo weekend iliyopita.

Mwimbaji huyo na mume wake Erwin Bach wamekuwa wakiishi pamoja kama mke na mume bila kuoana kwa miaka 18 mpaka wikendi iliyopita walipoamua kuhalalisha ndoa yao iliyohudhuriwa na watu maarufu akiwemo Oprah.

Kwa mujibu wa TMZ ripoti zinasema jumla ya watu 120 walihudhuria sherehe hiyo.

Hii ni ndoa ya pili kwa Tina Tunner baada ya kuachana na mume wake wa kwanza Ike Turner mwaka 1978

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents