Habari

Tip Top Connection yaanzisha kitengo cha filamu, yasaka waigizaji watakaokuwa chini yake

Msanii wa kundi la Tip Top connection Tunda Man ametangaza kuwa kundi hilo kwa sasa limegawanywa katika sehemu mbili, muziki na filamu na kwamba kupitia kitengo cha filamu wanatafuta wasanii wenye vipaji vipya vya kuigiza na kujiunga na kundi hilo ili wafanye kazi chini ya kundi hilo.
tundaman
Tunda Man ameiambia Bongo5, “Tip Top connection inahitaji waigizaji wenye vipaji ili wafanye kazi chini ya kundi.”

Ameongeza kuwa kama kuna watu watakaopenda kushiriki na kujiunga na kundi hilo kwa upande wa uigizaji wa filamu wafikae mapema katika maskani ya Tip Top maeneo ya Magomeni, Dar es Salaam Jumapili hii tarehe 24/02/2013 asubuhi kwa shughuli nzima za usajili ambapo mkurugenzi mkuu wa shughuli hiyo ni mwanadada Sajenti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents