BurudaniHabari

TMK Wanaume kuzindua Kazi Ipo leo

TMK WanaumeKUNDI la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume au Wanaume Family lenye maskani yake Temeke, Dar es Salaam, leo litatambulisha wimbo wake mpya uitwao Kazi Ipo. [Listen to the track here]

TMK WanaumeKUNDI la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume au Wanaume Family lenye maskani yake Temeke, Dar es Salaam, leo litatambulisha wimbo wake mpya uitwao Kazi Ipo.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Meneja wa kundi hilo Said Fela, alisema utambulisho huo utafanyika kwenye ukumbi wa Club Bilcanas, Dar es Salaam.

“Tunautambulisha wimbo wetu wa Ipo Kazi, naamini mashabiki watapenda kujua nini ambacho vijana wamekifanya,” alisema Fela.

Hatua ya kutoa wimbo huo imekuja karibu mwezi mmoja, baada ya mmoja wa wasanii waliokuwa wanaounda kundi hilo Juma Kassim ‘Sir Nature’ kujiengua pamoja na wasanii wengine watatu.

Wasanii hao ni Francis Martin ‘Dolo’, Doto Makala ‘D-Chief’ na Kalama Bakari ‘Luteni Kalama’.

“Hatutaki maneno, ila kazi ndiyo itazungumza, sina cha kuzungumza kuhusiana na suala lolote lile, ila TMK Wanaume tupo, tunaendelea na makamuzi,” alisema Fela.

Kundi hilo Septemba 8 mwaka huu, lilifanya onesho maalumu la miaka minne tangu lianzishwe, ambapo lilifanyika ukumbi wa PTA uliopo Uwanja wa Maonesho wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki wa burudani.

Tamasha hilo lilikwenda sanjari na uzinduzi wa albamu za wasanii watatu ambao ni Sir Nature, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’ na Rashid Ziada ‘KR’. Albamu hizo ni History ambayo ni ya Nature, Ipo Siku (Temba) na Kamua kwa Uweza (KR).

Kundi la TMK Wanaume Family lilianza rasmi Septemba 16, 2002 mjini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa albamu ya Juma Nature iitwayo Ugali na hadi sasa limejijengea umaarufu katika albamu zake mbili ilizotoa ambazo ni Kutokea Kiumeni na Ndio Zetu.

Wasanii waliobaki katika kundi hilo baada ya Sir Nature kujiengua na wenzake ni Said Chege, Rashid Ziada ‘KR’, Yesaya Ambukile (YP), Yassin Habib (Y-Dash), Mzimu Abdul, Abdul Malipo na Salum Khalid ‘Stico’.

Press play to listen to the song “Kazi Ipo”:
{mmp3}angular2.swf|kazi ipo.mp3{/mmp3}

Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:6}


Bongo5.com brings you the latest news from East Africa at your finger tips. If you have a story you’d like to share please send an email to [email protected]

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents