Tobaa Michael Jackson!

Tobaa Michael Jackson!
Daktari wa magonjwa ya ngozi wa mfalme wa muziki wa Pop duniani,
Michael Jackson ameshindwa kukana uwezekano wa yeye kuwa baba mzazi wa
watoto wawili wa Michael Jackson, lakini pia akieleza hajawahi kumpatia
dawa ambazo ni hatari

Mtaalamu huyo Arnold Klein alibainisha hayo kwenye mahojiano
aliyofanya juzi na kituo cha televisheni cha ABC katika kipindi chake
cha Good Morning America, ambako pia alikana madai mengine kuwa yeye ni
mmoja wa madaktari ambao wanachunguzwa na Polisi wa Los Angeles
kuhusiana na kifo cha mfalme huyo wa Pop kilichotokea Juni 25 mwaka
huu.

Klein alibainisha hayo wakati akijibu swali la mtangazaji Diane
Sawyer, endapo yeye ndiye baba wa watoto wa Jackson, ambapo alishindwa
kukanusha hivyo kufanya kuwepo uwezekano wa yeye kuwa baba wa kweli wa
watoto hao. Tuhuma kuwa Klein anaweza kuwa baba mzazi wa watoto wawili
wakubwa wa Jackson kutokana na aliyewahi kuwa mke wa Jackson, Debbie
Rowe ambaye ndiye mama wa watoto hao, alikuwa anafanya kazi kwa daktari
huyo kwa miaka 23.

Watoto wa Michael Jackson

Watoto wa Michael Jackson

"Kwa uelewa wangu ninachoweza kusema ni kuwa mimi sio baba wa
watoto hao, lakini nakuambia wewe endapo shinikizo zaidi zitazidi
kujitokeza sitaweza kusema chochote kuhusiana na jambo hilo, " alisema
Klein. Alisema hawezi kujibu swali hilo kwa njia nyingine yoyote ile,
kwa sababu hataki kuendeleza uendawazimu ambao unaoendelea kusambaa
kuhusiana na suala hilo la watoto.

Pia alikataa kusema endapo anafikiri mwanamama Rowe aombe kupewa
dhamana ya kuwatunza watoto hao wawili badala ya mama yake Michael
Jackson, Katherine Jackson. "Siwezi kutoa majibu ya suala hilo, kwa
sababu kusema alitakiwa awe ama anataka iwe hivyo ni masuala mawili
tofauti," alisema Dk. Klein. Katherine Jackson alipewa dhamana ya muda
kuwatunza watoto hao siku chache baada ya kifo cha mwanae.

Rowe pia anafikiri naye aombe dhamana upya kuwatunza watoto wake
ama kupewa ruksa ya kuwatembelea, wakili wake alibainisha hayo mwishoni
mwa wiki iliyopita. Dk. Klein pamoja na kushindwa kuweka wazi suala
hilo la kuwa baba wa watoto hao wa Jackson, akitoa ufafanuzi juu ya
suala la yeye kutowahi kumpatia dawa hatari mfalme huyo wa pop, alisema
yeye ndiye alikuwa mtu aliyekuwa akizuia Jackson kupewa dawa hatari na
kubainisha kuwa siku tatu kabla ya kifo, mfalme huyo wa pop alifika
ofisini kwake huko Beverly Hills na hakuwa katika maumivu yoyote
makali.

Alisema Jackson alipofika ofisini kwake, hakuonyesha dalili zozote
kwamba alikuwa anasumbuliwa na jambo lolote: “Hakuwa na tatizo katika
kuzungumza, kutembea au chochote kile sikuona chochote kile ambacho
kingenifanya nipatwe na wasiwasi,” alisema na kuongeza kuwa siku zote
alikuwa na shaka na madaktari wengine wa Jackson.

Klein alisema:"Tatizo la Michael ni kwa sababu alikuwa tajiri hivyo
chochote alichotaka walikuwa wakimpatia". Pia alisema kuna wakati
alimshauri kutotumia dawa inayojulikana kama Dilaudid ambayo ina nguvu
mara 10 ya dawa aina ya Morphine. "Nilimwambia kuwa huwezi kuitumia
hiyo ni sumu zitupe kwenye pipa la takataka, lakini siwezi kuwa naye
kila wakati kumshauri namna hiyo," alisema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents