Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Toka nimeanza muziki hajawahi kutoa ngoma mbaya – Kala Jeremiah

 

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Kala Jeremiah amesema tangu ameanza muziki hajawahi kutoa ngoma mbaya.

Kala ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kijana’ amesema kuwa kuna baadhi ya nyimbo unazikia kwenye radio anaona kuna baadhi ya vitu vimepungua ila kwake hilo halijawahi kutokea.

“Mimi ni moja kati ya wasanii wachache sana toka wameanza muziki hajawahi kutoa ngoma mbaya, kama mtu haamini achukuae albamu yangu inatwa Pasaka ina nyimbo 23 asikilize wimbo baada ya wimbo atajua kwamba, mimi sijawahi kubahatisha wala kutoa ngoma mbaya” Kala ameiambia Bongo5.

Katika hatua nyingine amezungumia wimbo ‘Vijana’ kwa kusema ana uweka level moja na ngoma kama ‘Wana Ndoto’ lakini siyo Dear God kwa sababu kwake ni wimbo wa kawaida ingawa ulimtambulisha zaidi yeye kama msanii.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW