Technology

Toleo jipya la TECNO CAMON15 ina kamera yenye MP64 kutatua changamoto zote za kupiga picha

Toleo jipya la TECNO CAMON15 ina kamera yenye MP64 kutatua changamoto zote za kupiga picha

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO iliandika historia Tanzania kwa kuzindua simu yake mpya ya CAMON15  mwezi Aprili 15 mwaka huu kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Katika uzinduzi huo afisa masoko wa TECNO mtandaoni Bi. Salma Shafi amesema hii ni fursa kwa kampuni hiyo kuwasiliana na wateja wake na watanzania wote kwa ujumla kupitia teknolojia ya intanteti.

“Hii sio tu nafasi nzuri kwa TECNO kuwasiliana na wateja wetu na Watanzania moja kwa moja, lakini pia inamaanisha kuwa matumizi ya vifaa vya kielektroniki na teknolojia Tanzania yanakuja katika hatua mpya sawa na simu tutakayoizindua CAMON15 ambayo ina teknolojia mpya ya kisasa kabisa ambapo wateja wetu wataweza kushuhudia uzuri wake” alisema Bi. Shafi.

Wakati wa uzinduzi huo TECNO ilitambulisha rasmi toleo la simu yake mpya ya CAMON15 pamoja na teknolojia yake ya kisasa iliyotumika kutengeneza kamera hiyo pamoja na sifa nyinginez

Mwonekano wa TECNO CAMON 15

TECNO ambayo ni kampuni kinara yenye teknolojia ya juu katika tasnia ya smartphone, imekuwa kipaumbele katika kuwapandisha viwango wateja wake kwa kutoa matoleo mbalimbali ya simu zake kulingana na mahitaji. Hata hivyo toleo hilo jipya la CAMON15, kampuni hiyo imeweka kamera yenye MP64 nyuma huku ikisaidiwa na kamera nyingine ndogo mbili ili kuongeza ufanisi zaidi katika suala la picha.

Kamera ya TECNO CAMON15 ina teknolojia iliyojikita katika kutatua changamoto za kupiga picha kwenye maeneo yenye mwanga hafifu au usiku. Kamera hii imeondoa ama imejengewa uwezo wa kuvikabili vizuizi vyote ambavyo hufifisha picha, kutokana na teknolojia hii, picha iliyopigwa na CAMON15 inabaki kuwa bora hata ikikuzwa (zoomed) mara nane.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents