Habari

Toni Braxton avishwa koti la kiume jukwaani baada ya kivazi chake kuachia sehemu ya makalio (Video)

Nyota wa ‘Unbreak my heart’ Toni Braxton amejikuta katika wakati mgumu alipokuwa akitumbuiza jukwaani, baada ya nguo aliyokuwa amevaa kupata hitilafu na kumuacha wazi sehemu ya makalio kwa muda mrefu bila kugundua.

Toni-2

Kuna ule usemi kuwa usilolijua ni sawa na usiku wa giza, ndicho kilichomtokea Braxton wakati wa onesho lake la hivi karibuni huko New Jersy, Marekani pale ambapo staa huyo mkongwe bila kufahamu kuwa nguo yake imemuacha wazi sehemu ya makalio kwa muda aliendelea kuimba na kucheza mbele ya maelfu ya mashabiki ambao walikuwa wakimshangilia.

Picha ilianzia wakati Toni anaimba hit yake ya mwaka 2000 ‘He wasn’t man enough’ ndipo kigauni chake kilitereza upande wa nyuma na kusogea chini, na kusababisha makalio yabaki nje na g-string yake kuwa hadharani.

Toni mwenye miaka 45, bila kujua kilichokuwa kinaendelea katika mwili wake aliendelea kuwatumikia mashabiki wake waliolipa viingilio ili kupata burudani. Kibaya zaidi hakuna mtu aliyejitokeza kumpa taarifa ya kilichokuwa kinaendelea kwenye nguo yake.
Waimbaji wawili wasaidizi waliokuwa na Toni jukwaani walionekana kugundua kuwa boss wao yuko uchi kwa nyuma lakini tatizo likawa wanaanzaje kumpa ishara na wako jukwaani?

Toni-1

Baada ya dakika kadhaa za Toni kundelea kuperform katika hali hiyo huku akizidi kuwafaidisha mashabiki kwa kugeuka na kuwapa mgongo, ilifika muda akaruhusu baadhi ya mashabiki wapande jukwaani kuimba naye, (kumbuka mlango wa nyuma bado ulikuwa wazi), walipanda baadhi ya wanaume lakini nao hakuna aliyepata jeuri ya kumwambia kuwa nguo yake imedondoka na kumwacha wazi.

Hatimaye Toni mwenyewe akajishtukia kuwa hali sio shwari kwenye mwili wake na kuanza kuivuta nguo yake kwa kutumia mkono mmoja na mwingine kashika microphone akiimba na kucheza na wale mashabiki waliopanda jukwaani.

Toni-3

Baada ya kuhangaika kuvuta nguo yake bila mafanikio ndipo shabiki mmoja wa kiume kati ya wale waliokuwa wamepanda jukwaani alijitolea koti lake na kumvisha Toni likamsaidia kumsitiri sehemu iliyokuwa inabaki wazi. Hakika huyu jamaa alikuwa ni ‘Man enough’ wa Toni kwa usiku ule.

Muda mfupi tu baada ya kuvishwa koti msaidizi wake naye akaja kwa nyuma yake na kuanza kuirekebisha nguo yake, kumbuka wakati huo wote Toni anaendelea kuimba lakini alionekana kabisa kuvurugwa na hali ile.

Aliongezeka msaidizi mwingine wa Toni kurekebisha nguo kwa nyuma lakini zoezi likashindikana. Ndipo yule msaidizi wa kiume kuamua kumvua nguo yote hapo hapo jukwaani na kumuacha akiwa na lile koti pamoja na g-string kisha nguo yake ikapelekwa kusiko julikana na akamaliza show akiwa na koti la yule shabiki wake.

Tazama mwenyewe tukio zima lilivyokuwa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents