Michezo

Top 10 ya wafungaji Ligi Kuu Bara, VPL 2017

Ligi kuu soka Tanzania Bara inaelekea ukingoni kwa vilabu vingi yakisalia michezo miwili na baadhi kusalia na michezo mitatu na hivyo kudhihirisha kuwa sasa Meli ya ligi hiyo inaelekea kutia nanga punde na kushusha abiria wake, ambapo katika abiria hao wapo watakao fika salama katika safari hiyo nawapo baadhi ya abiria hao kutofika salama.

Kwa watakaoshindwa kufika salama, watakuwepo tena katika safari ijayo ya ligi kuu na badala yake wadau na mashabiki wa soka watashuhudia timu npya zikishiriki katika ligi hiyo, baada ya hapo Jana kushuhudia mchezo muhimu kwa klabu ya Yanga na katika mbio zake za kutetea ubingwa wake wa ligi kuu nchini.

Katika mchezo huo, wachezaji wa Yanga, Simon Msuva na Obrey Chirwa Kufunga magoli katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar na kuongeza idadi ya Magoli Ligi Kuu, Kwa ushindi huo Kumewafanya wachezaji hao kumzidishia Presha mchezaji Shiza Kichuya ambaye amekuwa hana mwendelezo mzuri wa Kufunga katika mzunguko huu wa pili wa Ligi.

Mpaka sasa Msuva anaongoza akiwa na Bao 13 sawa na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, huku Obrey Chirwa akiwa amefikisha mabao 11 ambayo ni sawa na mabao ya Shiza Ramadhan Kichuya, Abdulrahman Mussa na Simon Msuva wanaoongoza Kwa kupachika Mabao Mengi zaidi.

Wanaoongoza kwa ufungaji Magoli Ligi kuu ya Vodacon. 

  1. Abdulrahman Mussa mcezaji wa  (Ruvu JKT)  magoli- 13 anashika nafasi ya kwanza.

   2. Simon Msuva mchezaji wa klabu ya (Yanga) magoli – 13,
        3. Shiza Ramadhani Kichuya mcezaji wa klabu ya (Simba Sc) mago-11
     4.Obrey Chirwa mchezaji wa klabu ya  (Yanga) magoli -11

  1. Mbaraka Yusuph mchezaji wa klabu ya (Kagera Sugar) magoli  -11

Wengine ni

6. Amis Tambwe (Yanga)-10

7. John Bocco (Azam Fc)-9

8.Donald Ngoma (Yanga)-8

9.Rafael Daudi (Mbeya City ) – 8

10.Laudit Mavugo (Simba) – 7

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents