Burudani

Top Band VS Chidi Beenz safi sana!

Top Band VS Chidi Beenz safi sana!Matamasha mbali mbali hufanyika nchini lakini idea ya kuandaa tamasha la Hip vs Bongo Fleva ni ya aina yake ambapo unaweza kuona jinsi wasanii wa Top  Band walivyoweza kuungana na msanii Chidi Beeeenz na kufanya makamuzi ya aina yake katika ukumbi wa Dar West maeneo ya Tabata.

Top Band VS Chidi Beenz safi sana!

 

Matamasha mbali mbali hufanyika nchini lakini idea ya kuandaa tamasha la Hip vs Bongo Fleva ni ya aina yake ambapo unaweza kuona jinsi wasanii wa Top  Band walivyoweza kuungana na msanii Chidi Beeeenz na kufanya makamuzi ya aina yake katika ukumbi wa Dar West maeneo ya Tabata.

 

 

 

Bongo5 iliweza kuibuka ukumbini hapo ambapo ilishuhudia jinsi ambavyo bendi hiyo ilivyowakamata wakazi wa maeneo hayo kutokana na show ya hatari ambayo waliifanya ukumbini humo “hii ni mara yetu ya kwanza kufanya maonesho katika pande hizi lakini sio ishu wala si umecheki mwenye umati unavyoukubali mziki wetu? Alisema Daz Baba ambaye anasimama kama Rapa wakutumainiwa katika Bendi hiyo.

 

 

 

Top Band iliuchengua umati ulioibuka ukumbini hapo walipokuwa wakipiga kopi za ngoma mbali pamoja na nyimbo zao ambazo ziliwafanya mashabiki kushindwa kutulia kwenye viti vyao.

 

 

 

Sura ya mchezo ilibadilika kabisa pale msanii Chidi Beenz alipopanda jukwaani na kuanza kufanya mitindo huru (free style) ambazo zilikuwa ni za ukweli huku katika mashine Dj D-White akiendelea kufanya balaah ambapo alikuwa akienda sambamba na Chidi inavyotakiwa “yaani haina cha tabata wala wapi hapa mi nakamua tu” alisema D-white huku akiendelea kubofya machine yake.

 

 

 

Kwa kifupi hakuna msanii aliyecheza chini ya kiwango Top Band walijipanga inavyotakiwa halikadhalika Chidi nae aliweza kufanya kweli kwa upande wake pia.

 

Unaweza kuanagalia videoclip za Top Band na Chidi Beeeenz wakikamua live kwa kubofya hapa!!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents