Habari

Top C Agonganisha Wapenzi Wake


Msanii Top C ambaye ni maarufu kwa nyimbo ya “Sababu Ya Ulofa” anasemekana kupata tafrani ya aina yake baada ya wapenzi wake wote wawili kukutana nyumbani kwa wazazi wake baada ya msanii huyo kupata ajali na kukimbia alikopanga akihisi amemkimbia mmoja wapo na kwenda kwa wazazi wake kabla ya wapenzi hao kufumaniana huko huko.
Ishu ilitokea pale wapenzi hao walipokwenda nyumbani kwa wazazi wake kila mmoja kwa wakati wake ambapo kila mmoja alikuwa amekwenda nyumbani kwa wazazi wa Top C kama mpenzi wa Top C na kujikuta wote wawili wamepiga kambi kwa msanii huyo.
Inavyosemekana baada ya Top C kujua ni lazima atatembelewa na kina dada hao aliomba kutokwenda kuishi kwenye nyumba aliyopanga kwani wapenzi hao wote wawili wanapajua hivyo akaona ni afadhali aende kwa wazazi wake.
Waswahili wanasema la kuvunda halina ubani ikatokea kama ajali vile wapenzi hao wakakutana na kuleteana tifu ambapo inasemekana mmoja wao alimpiga kibao na kuondoka zake. Hata hivyo msanii huyo akiongea na Sudi Brown alithibitisha tafrani hilo kumtokea lakini anasema ameyatatua mambo hayo…

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents