Uncategorized

Top Fleva watoa sababu ya kufanya wimbo unaofanana na wa P. Square Beautiful Onyinye


Baada ya kuwa kimya kwa muda kundi la Top Fleva wakaamua kutoa ngoma “Rudi home” ambayo imekaa kama remix ya wimbo wa P. Square “Beautiful Onyinye”.

Bongo5 ilifanya mahojiano na kiongozi wa kundi hilo Tony, ambaye alisema uamuzi uliowasukuma kufanya kitu kama hicho siyo kwamba wameishiwa vitu vya kufanya, bali walikuwa wamekaa na bosi wao ghafla wimbo huo wa P.square “Beautiful Onyinye” ukawa unapigwa bosi wao akasema huu wimbo umetengenezwa vizuri sana, tukamjibu mbona tunaweza tukafanya kitu kama hicho, basi sisi tukafanya kitu kama hicho katika studio ya shebizo records.

“Huu wimbo hauko kibiashara tumejipima, kuna kazi zetu zinakuja kaeni mkao wa kula” alisema Tony wa Top Fleva.

Sikiliza hapa Rudi Home wa Top Fleva
Download Here

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents