Aisee DSTV!

Toronto Raptors waukaribia Ubingwa wa NBA, wawatembezea kipigo mabingwa watetezi Golden State Warriors, wahitaji ushindi wa mechi moja pekee kubeba taji hilo

Timu ya Toronto Raptors imezidi kujikita katika nafasi nzuri kwenye fainali za ligi ya mpira wa kikapu maarufu kama basketball nchini Marekani (NBA) baada ya alfajiri ya leo kuwatembezea kipigo mabingwa watetezi Golden State Warriors kwa jumla ya pointi 105-92.

Huo ulikuwa ni mchezo wa nne katika mfululizo wa fainali hizo za NBA unaowafanya vijana wa Toronto kuongoza kwa michezo 3-1.

Kwa matokeo hayo timu ya Toronto Raptors mpaka sasa inahitaji kushinda mechi moja pekee kati ya michezo mitatu iliyosalia ili kutangaza ubingwa wa ligi hiyo msimu huu. Mchezo wa tano utapigwa alfajiri ya Juni 11, 2019 ambapo Warriors watakuwa ugenini.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW