Michezo

Torres Atetewa

Kocha wa Liverpool Roy Hodgson ameibuka na kumtetea Fernando Torres baada ya mchezaji huyo kudaiwa kutokujituma uwanjani. Lawama kwa Torres ziliibuka baada ya kushindwa kung’ara katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Birmingham kwenye uwanja wa Mtakatifu Andrew na pia kutokana na suluu mmoja aliyemshambulia Torres.

Mchezaji wa zamani wa Liverpool Jamie Redknapp alikuja juu na kudai kuwa hakuwajibika kama ilivyotarajiwa katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili.

Lakini Hodgson amesema,Torres ailyekuwa mmoja wa wachezaji wa Hispania waliotwaa ubingwa wa Dunia mwaka huu atakua poa. ‘Sikuona tatizo siku ile, Torres anajituma na kucheza kwa ustadi, alisema Hodgson.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents