Michezo

Tottenham yampa siku za mapumziko Adebayor kwa kuweka wazi kuwa aliwahi kufikiria kujiua mara nyingi!

Emmanuel Adebayor amepewa ruhusa ya kupumzika na klabu yake ya Tottenham baada ya kuweka wazi kuwa aliwahi kufikiria kujiua.

Manchester-United-v-Tottenham

Tayari hatokuwepo kwenye mechi ya mwisho ya msimu huu Jumapili hii dhidi ya Everton na hatokwenda kwenye ziara ya baada ya msimu na klabu yake Malaysia na Sydney.

Mchezaji huyo wa Togo amefanya mazungumzo ya dharura na klabu yake baada ya hivi karibu kuandika mfululizo wa post za Facebook kuhusu ugomvi na familia yake.

Kwenye post ya tatu jana alieleza jinsi alivyowahi kufikiria kujiua mara nyingi kutokana na masuala ya kifamilia.

“Many times I wanted to give up. Ask my sister Iyabo Adebayor how many times I have called and was ready to commit suicide? I kept these stories for years… But If I die, no one would know my story, no one would learn from it… Some people say I should keep these stories private, but someone has to sacrifice himself; someone has to talk about it,” ameandika Adebayor kwenye maelezo hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents