Burudani

Tour ya ‘OTRII’ yaacha gumzo nchini Poland, Beyonce ashuka jukwaani kwa kutumia ngazi (+video)

Ziara ya muziki ya ‘OTRII’ ya wanamuziki wawili wakubwa duniani ambao pia ni mtu na mkewe, Jay Z na Beyonce usiku wa kuamkia jana imeacha gumzo jijini Warsaw nchini Poland baada ya jukwaa walilokuwa wakitumbuiza kupata hitilafu.

Image result for beyonce fails stage warsaw
Mrembo Beyonce akishuka jukwaani kwa ngazi baada ya mitambo kuharibika

Video hiyo inayomuonesha Beyonce akiwa na timu nzima ya OTRII jukwaani wakimshinikiza ashuke jukwaani kwa kutumia ngazi imeanza kusambaa mitandaoni tangu siku ya jana.

Hata hivyo, Beyonce alifanikiwa kushuka salama kwenye nguzo hiyo inayokadiriwa kuwa na urefu wa futi 10 hadi 15 na show ilimalizikia hapo.

Leo Beyonce na Jay-Z wanatarajiwa kutumbuiza nchini Ujerumani kwenye ziara hiyo ya Muziki ya On The Run II, Tazama video ya show hiyo hapa chini hadi Beyonce alipopatwa na majanga hayo jukwaani.

https://youtu.be/Rh3WDuv9qF4

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents