Technology

Toyota kuzindua magari yanayopaa kwenye Olimpiki mjini Tokyo

Kampuni ya utengenezaji magari ya Toyota, ambayo imefadhili utengenezaji wa gari inayoruka angani ikiwa ni mradi uitwao Cartivator Project, yamepanga kuzinduliwa mwaka 2020 katika mashindano ya Olimpiki.

Watengenezaji wa magari hayo wanatarajia kuyakamilisha mwishoni mwa 2018 na yataonekana katika mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika katika mji wa Tokyo.

Gari hiyo ambayo imepewa jina la Skydrive itakuwa na matairi matatu na propeller nne ambapo pia itakuwa ikisafiri umbali wa mile takribani 62 kwa saa ikiwa angani kwenye urefu wa futi 32.8.


Picha ya gari hilo litakapokuwa angani

Toyota imewekeza kiasi cha dola milioni 350 katika mradi huo ambao umebuniwa na kundi la maengineer vijana waliopo kwenye shule ya Aichi Prefecture.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents