Burudani

TPF5 wazindua album ya Top 10


Kampuni ya East Africa Breweries pamoja na universal Music Group waliandaa hafla maalum ya kuzindua album ya Tusker Project Fame Season 5 Top Ten, ambayo ilifanyika jana usiku katika hoteli ya kitalii Tribe jijini Nairobi.

Hafla hiyo, ambayo pia iliwajumuisha mastaa kibao wa Tusker project Fame zilizopita iliandaliwa na kampuni ya matukio ya Homeboyz Activate na kuhudhuriwa pia na washiriki wa Tusker Project Fame season five ambayo ilimalizika mwezi wa nane mwaka huu.

Kwa mujibu wa mdau wetu aliyepo jijini Nairobi, hafla hiyo ilianza majira ya saa kumi na mbili na nusu kwa Cocktail ya nguvu kabla ya wasanii Steve, Samantha, Jackson, Nancy, Allan, Eunice, Sharon na Ruth Matete kuwasili wakiongozwa na mwalimu Mkuu wa sasa wa academy ya Tusker Project Fame Hellen na kuashiria kuanza rasmi kwa uzinduzi huo.

Wasanii hao ambao wote walionekana wakiwa na nyuso za furaha waliimba baadhi ya nyimbo ambazo ziko kwenye album hiyo na kurudisha hisia za wakati wakiwa katika mashindano hayo katika misimu iliyopita.

Hafla hiyo ilianza na tukio la kusikiliza nyimbo zote kumi na kila msanii moja moja kupewa nafasi ya kuelezea nyimbo yake ambapo mc wa tukio hilo Mtangazaji wa Homeboyz Radio Jeff Motte aliongoza kuuliza maswali hayo.

Baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika Album hiyo ni pamoja na Avec Toi (Samantha), This Guy(Nancy welele), I will be there 9 steve), sio Mapenzi ( Jackson) na Ndoto Langu iliyotungwa na kuimbwa na Ruth Matete.

Mdau wetu alihabarisha kuwa baadhi ya washiriki wa Tusker project Fame 5 hawakufika katika hafla hiyo, hao ni pamoja na Doreen na Joe ambao wote walikuwa washindi namba mbili na tatu katika msimu wa Tusker season 5.

Baadhi ya wadau na mastaa wa muziki na burudani waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na watangazaji wa Kiss Fm wakiongozwa na Shaffie Weru, Prodyuza na msanii Collo, mtangazaji Ian Mugoya, Dj Hassan, watangazaji wa Radio Capital Fm wakiongozwa na Vincent Ochieng, waandishi wa habari pamoja na viongozi waandamizi wa kampuni ya East Africa Breweries na Universal Music Group.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents