Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

TPLB yanogesha zawadi ya mchezaji bora wa mwezi VPL

Bodi ya ligi (TPLB) imeikishirikiana na wadhamini wameboresha zawadi za mchezaji bora wa mwezi wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi za TFF, Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi hiyo, Boniface Wambura amesema kwa sasa mchezaji huyo bora atakuwa akipokea tuzo maalum, fedha taslim shilingi milioni moja pamoja na king’amuzi cha Azam TV.

Afisa huyo wa TPLB amesema zawadi zilizoongezwa ni tuzo itakayokuwa ikitolewa na bodi hiyo pamoja na king’amuzi ambacho kitakuwa kikitolewa na wadhamini wa ligi hiyo upande wa matangazo ya runinga Azam TV, huku shilingi milioni moja iliyokuwepo tangu awali itaendelea kutolewa na wadhamini wakuu wa ligi ambao ni Vodacom Tanzania.

Wambura ameongeza kuwa tayari zawadi hizo mpya zilizotangazwa leo zimeanza kutolewa kwa aliyekuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba, Mudhathir Yahya kutoka Singida United na kesho (Januari 11, 2018) mchezaji bora wa mwezi Disemba 2017 anatarajia kutangazwa.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW