Habari

TRA yakusanya shilingi trilioni 10.87 kwa miezi 9

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ripoti ya mapato yaliyokusanywa ndani ya miezi 9 kuanzia June 2016 hadi March 2017 ambayo ni Shilingi Trilioni 10.87 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.99 ukilinganisha na mwaka uliopita.


Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo alisema zaidi ya Shilingi Trilioni 1.34 zilikusanywa katika mwezi March 2017 pekee ikionesha kupanda kwa asilimia 2.23 ukilinganisha makusanyo ya mwezi kama huo mwaka 2016 ambapo zilikusanywa Shilingi Trilioni” 1.31.

“Katika kipindi cha miezi 9 ambayo imeanzia mwezi wa June 2016 hadi mwezi Marchi 2017, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Trilioni 10.87 za Kitanzania hayo ni makusanyo ya miezi tisa,”alisema Kayombo.

Aliendelea kufafanua kuwa, “Katika mwezi wa Machi 2017 TRA imekusanya jumla ya shilingi trilioni 1.34 ukilinganisha trilioni 1.31 ya mwezi machi 2016 ambayo ni sawa na aslimia 2.23. Pamoja na mafanikio tuliyoyapata katika kipindi cha miezi tisa iliyopita, katika kipindi cha miezi mitatu kilichobaki TRA itahakikisha inakusanya kodi mbalimbali ili kufikia lengo la kukusanya trilioni 15.1 kwa mwaka.”

Aidha Katika hatua nyingine, Kayombo amesema TRA inaendelea na mpango wake wa kukusanya kodi za majengo kwa kutoa viwango maalumu vya kodi kwa majengo ambayo bado hayajafanyiwa tathimini.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents