Burudani

Trailer: Mkenya, Lupita Nyong’o aigiza kwenye filamu ya action ya Liam Neeson, Non-Stop

Baada ya kuigiza na Brad Pitt kwenye filamu ya Hollywood ya ‘12 Years A Slave’ muigizaji wa Kenya, Lupita Nyong’o amepata shavu jingine.

Msichana huyo mwenye miaka 30 ataonekana kwenye filamu ya Liam Neeson, Non-Stop itakayoingia sokoni February 2014. Filamu hiyo ya action inatokea kwenye safari ya ndege kutokea New York kwenda London, Uingereza.

Lupita
Lupita akiwa ndani ya ndege, kwenye filamu ya Non-Stop

Wakati wa safari hiyo, mwanajeshi wa angani wa Bill Marks (Neeson) anapokea mfululizo wa jumbe za simu zinasema kuwa abiria mmoja kwenye ndege hiyo atakuwa akiuawa kila baada ya dakika 20 mpaka kiasi cha dola milioni 150 kitatumwa kwenda kwenye akaunti ya benki ya siri.

Baada ya akaunti hiyo ya benki kugundulika kuwa ipo chini ya jina lake mwenyewe, Marks na bomu linapatikana ndani ya ndege hiyo, Marks anadhaniwa kuwa ni mtekaji.

Katika filamu hiyo Lupita ameigiza kama Gwen aliyekuwa mmoja wa abiria wa ndege hiyo, kama si mhudumu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents