Trending kwenye Twitter #Dear Nyerere

Leo tunatimiza miaka 13 tangu kifo cha hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia October 14, 1999.

Wakati watanzania wengi wakiitumia siku hii kumkumbuka shujaa huyo, kwenye mtandao wa Twitter watu wameanzisha topic iitwayo #Dear Nyerere ambayo wanaandika mengi ya kumwambia.

Hizi ni miongoni mwa tweets hizo:

#DearNyerere zile industries zilizokuwepo zimekufa karibu zote, siku hizi vijana ajira mpya ni ya kuokota makopo.

#DearNyerere rick ross alikuja Tz bhana”

#DearNyerere Hii Nchi imekwisha uzwa. Kuna watu walinenepa baada ya wewe kuvuta

#DearNyerere kuna chuo kimeanzishwa,kinaitwa Udom,ni kikubwa sana Africa na duniani..lakini tunafanyia registration uwanja wa Jamhuri.

#DearNyerere mtanzania akinunua tu kilo ya sukari ina mana hawezi kula siku nzima tena,tanaishi zaidi ya chini ya dola 1

#DearNyerere yule jamaa mwenye nywele nyeupe uliyemkataa kwenye uongozi baada ya kula pesa za vijana anajiandaa kugombea Urais

#DearNyerere Bei Ya Sukari Inafanya ninywe Chai Na Pipi arifee.

#DearNyerere naomba nitumie jina lako kama babu yangu nipewe cheo serekalini na katika chama,hata ubunge viti maalumu babuu

#DearNyerere UDSM imekua Chuo ya mambulula

#DearNyerere sasa hiv wanafunzi wa shule ya msingi wanafaulu sana ila hawajui kusoma ata kuandika!

#DarNyerere cku hz kuna madem facebuk na twitter wanajiita preciouz na wana sura kama goti la nyati

#DearNyerere hukuona aibu kukemea wafanyabiashara because ulikua sio mfanyabiashara. Unajua ikulu imekua sehemu ya kupiga dili? Dah.

#DearNyerere aliyeimba sihitaji marafiki ni @FidQ wakati we ulisema umoja na mshikamano kwanza
#DearNyerere alafu baba ulikosea sana kuwabadilishia hawa polisi suruali,ungewaacha na vikaptula vyao baba,wangeona aibu kuomba rushwaa

#DearNyerere vijana wengi tunaichukia CCM sababu inalea mafisadi naamini hata wewe ungekuepo ungerudisha kadi

#DearNyerere Ungejua ungefanya kingereza kiwe ndiyo lugha ya taifa kwani kina tusumbua sana hadi wabunge

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents