Habari

Treni ya Mwakyembe yasitisha kutoa huduma

Shirika la Reli Tanzania (TRL), limesitisha kutoa huduma ya treni kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kwa siku mbili kutokana na hitilafu kubwa iliyojitokeza kwenye kichwa kimoja cha treni.

treni

Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Mhandisi Kipallo Kisamfu, ilisema kuwa shirika hilo limelazimika kusitisha huduma za treni hiyo kwa siku mbili ili kupisha marekebisho ya kiufundi katika kichwa kimoja cha treni hiyo.

Akifafanua taarifa hiyo Kisamfu amesema kuwa Jumamosi iliyopita ndipo iligundulika kichwa kimoja kina tatizo linalohitaji marekebisho makubwa. Aliongeza kuwa treni hiyo hutumia vichwa vitatu katika utoaji wa huduma hiyo ya usafiri ambapo vichwa viwili hutumika moja kwa moja na kingine kimoja hutumika kama akiba.

Aliendelea kusema baada ya kugundua tatizo hilo kichwa hicho cha treni kilipelekwa katika karakana ya shirika hilo iliyoko Morogoro kwaajili ya matengenezo makubwa.

“Kutokana na kukosekana kwa kichwa cha dharura tumelazimika kusitisha huduma kwa muda na wahandisi wetu wa karakana yetu kuu ya Morogoro wanatarajia kukamilisha kazi hiyo kabla ya siku ya Jumatano hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza,” Alisema Kisamfu.

SOURCE: NIPASHE

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents