Burudani

Trevor Noah atangazwa kusherehesha tuzo za MTV MAMA

Mchekeshaji wa Afrika Kusini anayefanyika kazi nchini Marekani, Trevor Noah, ametangazwa kuwa mshereheshaji wa tuzo za mwaka huu za MTV MAMA.

cs2fwocukaaed35

Awali Idris Sultan, Basket Mouth (Nigeria), Idris Elba (Uingereza) na Kevin Hart (Marekani) walikuwa miongoni mwa washereheshaji wengine waliokuwa wanafikiriwa.

Tuzo hizo zitafanyika October 22, 2016, kwenye ukumbi wa Ticket Pro Dome, Johannesburg, Afrika Kusini. Yemi Alade, Ycee, Cassper Nyovest na Alikiba wanatarajiwa kuwasha moto kwa kutumbuiza.

14322422_10154084051863585_1296569323982964330_n

Rapper wa Afrika Kusini, Nasty C na muimbaji wa nchi hiyo, Babes Wodumo nao watatumbuiza. Majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo mwaka huu yatatajwa, jijini Johannesburg mwezi huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents