Habari

Trump aamrisha bendera ya Marekani kupepea nusu mlingoti

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa amri jana ya bendera kushushwa nusu mlingoti kwa siku tatu mfululizo, kuomboleza vifo vya Wamarekani waliokufa kutokana na virusi vya corona.

Trump announces three days of mourning for coronavirus victims and ...

Trump ameamrisha hatua hiyo, baada ya idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19 kukaribia 100,000 nchini humo.

Aidha Trump amesema bendera zitabakia nusu mlingoti Jumatatu ijayo ambayo ni Siku ya Mashujaa nchini humo, kuwakumbuka wale ambao wamepoteza maisha wakilitumikia jeshi la Marekani.

Ingawa idadi ya vifo vya kila siku nchini humo haikuongezeka, watu bado wanaendelea kupoteza maisha, na hesabu kamili inapindukia vifo 94,500 – likitajwa kuwa ni taifa lenye vifo vingi ulimwenguni. Wiki hii Marekani imerikodi vifo 1,300 kwa siku, vinavyotokana na virusi vya corona.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents