Habari

Trump adai utawala wake umefanya mengi zaidi kuliko zilizopita katika historia ya Marekani, watu waangua kicheko (+video)

Rais Donald Trump wa Marekani hapo jana amelihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa akigusia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na mafanikio ambayo Marekani imepata hadi sasa chini ya utawala wake.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la DW, Trump amesema utawala wake umefanya mengi zaidi kuliko tawala nyingine zilizopita katika historia ya Marekani kauli iliyosababisha kicheko kutoka kwa umati uliokuwa ukimsikiliza kwenye mkutano huo.

Trump pia alisema wanafanya vizuri katika suala linalohusiana na Korea Kaskazini na kumshukuru kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un , China , Korea Kusini na Japan kwa ushirikiananao.

Kwa upande mwingine rais huyo ameishutumu Urusi na serikali ya Syria kwa uhalifu uliofanywa dhidi ya raia nchini Syria.

Donald Trump hali kadhalika ametetea uamuzi wake wa kuiondoa Marekani katika makubaliano ya kihistoria ya nyukilia ya mwaka 2015.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents