Afya

Trump aipa WHO siku 30 kufanya mabadiliko “Walikuwa na uwezo wa kuidhibiti Corona”

Rais wa Marekani, Donald Trump amemtumia barua Mkuu wa Shirika la Afya duniani, (WHO) akitishia kuondoa kabisa mchango wa taifa lake kifedha kwa shirika hilo, kutokana na janga la Covid-19

Barua hiyo imeipa WHO siku 30 kufanya “maboresho makubwa” au ipoteze mamilioni ya dola na hata uanachama wa Marekani kwa pamoja.

Barua iliyoelekezwa kwake Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus inakosoa awamu mbalimbali za WHO za kushughulikia janga la corona tangu mwezi Desemba.

Bwana Trump pia amelituhumu shirika hilo la Umoja wa Mataifa (UN) kwa ”kibaraka wa China”.

Rais huyo anayekabiliwa na uchaguzi mwaka huu na yeye kukosolewa kwa namna anavyoshughulikia janga hilo, ameitupia lawama China kwa kujaribu kuficha taarifa kuhusu mlipuko wa virusi vya corona pia ameishutumu WHO kuwa kushindwa kuiwajibisha China.

Awali Waziri wa Afya wa Marekani pia aliitupia lawama WHO kuruhusu Covid -19 kushindwa kudhibitika kwa gharama ya maisha ya watu wengi.

”Shirika hili lilifeli kupata habari ambayo ulimwengu ulihitaji”, alisema waziri wa Afya wa Marekani Alex Azar.

Bwana Alazar alitoa matamshi hayo katika hotuba kwenye mkutano wa UN.

Mkuu wa WHO awali alikubali kufanyika uchunguzi ambao utaweka wazi jinsi shirika hilo lilivyoangazia mlipuko huo.

Dkt. Tedros amesema kwamba uchunguzi huru ambao utatazama mafunzo na kutoa mapendekezo utafanyika mapema.

Mkutano huo wa siku mbili – unaofanyika kila mwaka na unaohusisha nchini 194 wanachama wa WHO huangazia kazi ya shirika hilo na unajiri wakati ambapo kuna vita vya maneno kati ya china na Marekani kuhusu virusi hivyo.

Rais wa Marekani Donald Trump , ambaye anakabiliwa na uchaguzi mkuu mwaka huu ambaye amekosolewa jinsi anavyotatua ugonjwa huo nchini Marekani , amelaumu China kwa kujaribu kuziba mlipuko huo na kuilaumu WHO kwa kushindwa kuiwajibisha China.

Rais wa China Xi Jingpin , ambaye ametetea vitendo vya China wakati wa mlip[uko huo , alisema katika mkutano huo kwamba taifa lake lilikabiliana na ugonjwa huo kwa uwazi na kusisitiza kwamba uchunguzi wowote ufanyike baada ya mlipuko huo kudhibitiwa.

Aliongezea China itatoa $2bn katika kipindi cha miaka miwili ili kusaidia mataifa duniani na kutoa ombi la kugawanya chanjo itakapokuwa tayari.

Wakati huohuo rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema kwamba WHO inafaa kupewa uwezo wa kisheria kuhakikisha kuwa matafa yanaripoti milipuko na kupeana data.

Mlipuko mwengine hatari wa magonjwa ya maambukizi unaweza kutokea wakati wowote na ni muhimu tuweze kukabiiana nao haraka iwezekanavyo, alisema.

Zaidi ya watu milioni 4.5 wameambukizwa na zaidi ya 300,000 wamefariki tangu virusi hivyo kutokea chini China mwezi Disemba.

Grey line

Je ni kipi kinachozungumzwa katika mkutano huo?

Trump na AzarAlex Azar (kulia) na Rais Donald Trump wamezishambulia WHO na Uchina juu ya mlipuko wa corona

Muungano wa bara Ulaya , pamoja na mataifa ikiwemo Uingereza, Australia na New Zealand umekuwa ukisukuma uchunguzi kuhusu jinsi mlipuko huo ulivyoangaziwa na ni mafunzo gani watu wamejifunza.

Msemaji wa EU Virginia Battu- Henreiksson alisema kwamba maswali muhimu yanahitajika kujibiwa katika uchunguzi huo.

Ni vipi mlipuko huo ulisambaa? Je mlipuko huo ulisambaa kwa njia ipi? Vyote hivi ni muhimu kwetu sisi tukisonga mbele ili kuzuia kutokea kwa mlipuko mwengine wa aina hii. Hatahivyo , aliongezea kwamba sasa sio wakati wa kulaumiana.

Pendekzo la kutaka uchunguzi kufanywa linatahitaji kupigiwa kura huku thuluthi mbili zikihitajika kwa nchi wanachama ili kuweza kupita.

Mwezi uliopita ripoti ya EU ilishtumu China kwa kusambaza habari potovu kuhusu m;lipuko huo. Idara ya huduma ya Muungano huo ilisema kwamba Urusi na China kwa kiwango kidogo zilikuza dhana potofu.

Vilevile nchi wanachama zilikubaliana siku ya Jumatatu kwamba kuchelewesha mazungumzo ya kuipatia Taiwan jukumu la kuchunguza katika mikutano , huku Taipei ikisema itachelewesha mahitaji yake hadi baadaye mwaka huu.

China inayosema Taiwani ipo katika himaya yake imezuia kushiriki kwa Taiwana tangu 2016.

Katika majuma ya hivi karibuni , Marekani na Muungano wa Ulaya , Japan na mataifa mengine kadhaa yameunga mkono Taiwan kuwasilisha ombi la kutaka kushiriki katika mikutano hiyo.

Wakati wa mazungumzo ya Jumatatu , waziri wa maswala ya kigeni Mike Pompeo alisema kwamba kuiwacha nje Taiwan zaidi kunaharibu maadili ya WHO.

Je China inashutumiwa na nini?

China inasema kwamba woito wa kufanyika kwa uchunguzi utaondoa umakini wa kukabiliana na mlipuko wa coronaChina inasema kwamba woito wa kufanyika kwa uchunguzi utaondoa umakini wa kukabiliana na mlipuko wa corona

Mlipuko huo kwa mara ya kwanza ulianzia katika mji wa China wa Wuhan mwisho wa mwaka jana na ulidaiwa kuanzia katika soko moja la chakula.

Tangu wakati huo , wanasiasa wakuu wa Marekani wamesema kwamba chanzo cha ugonjwa huo ni maabara moja ya utafiti mjini Wuhan ambayo ilikuwa ikifanya utafiti wa virusi vya corona katika popo . China imekana wazo hilo.

Bwana Pompeo alisema mapema mwezi huu kwamba kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba virusi hivyo vilianzia katika maabara ya Wuhan.

Hatahivyo, katika mahojiano na runinga alionekana akirudi nyuma, akisema tunajua ulianza Wuhan lakini hatujui kuanzia wapi ama kutoka kwa nani.

Pendekezo hilo linazungumzia chanzo cha virusi hivyo na njia ambayo ugonjwa huo ulipitia hadi kuambukiza wanadamu.

Mwezi uliopita , mwanadiplomasia mkuu wa China Chen Wen aliambia BBC kwamba mahitaji ya uchunguzi yana msukumo wa kisiasa na kwamba hatua kama hiyo huenda ikaondoa umakini na rasilimali za kupigana vita dhidi ya corona.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents