Habari

Trump aisaidia Tanzania Trilioni 1.2

Serikali ya Marekani kupitia ofisi ya Rais Donald Trump imetangaza kuipatia Tanzania ufadhili wa kukabiliana na ongezeko la virusi vya ukimwi.

Tokeo la picha la Donald trump
Donald Trump

Marekani ambayo siku chache zilizopita ilitangaza kusimamisha ufadhili wake kwa wizara ya afya nchini Kenya, imeipa Tanzania kitita cha dola milioni 526 sawa na Shilingi trilioni 1.2 za Kitanzania.

Kitita hicho kutoka mfuko wa President’s Emergency Plan for AIDS Relief  (PEPFAR) kitatumika kufanikisha mpango wa kutoa huduma kwa zaidi ya watu milioni 1.2 wanaoishi na virusi vya vinavyosababisha Ukimwi.

Akizungumza baada ya tangazo hilo, mwakilishi wa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser amesema kuwa wanalenga kufanikisha kizazi kilicho huru kutoka virusi nchini Tanzania.

Kwa niaba ya raia wa Marekani, tunafurahia ushirikiano wetu na Tanzania na tunajitahidi kuhakikisha hakuna anyeachwa nje,” Amesema Virginia Blaser.

By Godfery Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents