Trump amfuta kazi bosi wa usalama wa shirika la uchaguzi aliyepinga madai yake

Rais Trump amesema “amemfuta kazi ” mkuu wa usalama wa mtandao na shirika la usalama wa miundo mbinu ya uchaguzi (Cisa) Chris Krebs kwa taarifa zake “zisizo sahihi kwa kiwango cha juu ” kuhusu maadili ya kura.

Bwana Trump amekataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa Marekani, akitoa madai yasiyo na ushahidi ya wizi “mkubwa ” wa kura

Maafisa wa uchaguzi wanasema kura ya mwaka huu ilikuwa “moja ya kura salama zaidi ” katika historia ya Marekani.

Wiki iliyopita Rais Trump alimfuta kazi waziri wa ulinzi Mark Esper, huku kukiwa na ripoti kwamba alikuwa na wasiwasi juu ya utiifu wa mkuu huyo wa Pentagon.

Kuna tetesi mjini Washington DC kwamba kabla ya Trump kuondoka madarakani mwezi Januari , Mkuu wa CIA Gina Haspel na mkurugeni wa FBI Christopher Wray huenda wakawa miongoni mwa wale watakaofutwa kazi na Trump.

Sawa na wengine wengi waliofutwa kazi na Bw Trump, Bw Krebs alifahamu kwamba amefutwa kazi alipoona tweet ya Trump Jumanne, licha ya kwamba alikuwa mtu wake wa karibu, kulingana na taarifa ya shirika la habari la Reuters.

Lakini baada ya kufutwa kazi, Mkurugenzi huyo mtendaji wa zamani wa kampuni ya hakuonekana kujuta.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW