Habari

Trump amjibu Jay Z baada ya kuitwa ‘Bakteria hatari’

Wakati Eminem alimpo mdisi Donald Trump wakati akiwa na BET na baadaye kwenye nyimbo kadhaa katika albamu yake iitwayo Revival, Rais huyo hakumjibu mahali popote kwenye vyombo vya habari vya kijamii au vinginevyo. Lakini Trump ameonekana kukerwa sana na kile alicho kisema Jay-Z.

Jay alifanya mahojiano na CNN kwenye kipindi kiitwacho “The Show Jones” Jumamosi ambapo alizungumzia juu ya ndoa yake na Beyonce, nafasi yake kama baba, madaraka ya Trump na mengi zaidi. Rapa huyo hakupendezwa na maoni ya Trump ya “shithole” mapema mwezi huu ambapo alisema “kimemuumiza sana na Kila mtu anahisi hasira lakini baada ya hasira hiyo ni maumivu kwa sababu ameongelea idadi kubwa ya watu na yeye hajui tu maeneo hayo yalivyo kuwa na watu wazuri.”alisema Jay Z.

Trump alisema maneno hayo katika mkutano mmoja hapo awali na alikataa mpango wa uhamiaji na kuwalinda washiriki wa DACA. “Why do we want all these people from sh*thole countries coming here?” Trump aliwaambia wajumbe siku ya jumatano Januari 11 mwaka huu. Jay-Z aliendelea kwakusema “Huondoi takataka bali unaendelea kunyunyizia chochote juu yake ili kukubalika na kisha unajua kama mambo hayo yanavyokua basi unatengeneza bakteria hatari na sasa tuna Donald Trump bakteria hatari.

Trump aliona maoni ya Jay-Z na kuamua kumjibu mapema Jumapili asubuhi. “Mtu yeyote tafadhali wajulishe Jay-Z kuwa kwa sababu ya sera zangu, ukosefu wa ajira kwa watu weusi kwa sasa upo katika hatua ya chini” Trump alitweet.

Bonyeza hapochini kutizama mahojiano yote ya Jay Z

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents