Burudani

“Trump amrithi Arsenal Wenger”:Piers Morgan

Mwandishi wa habari wa Uingereza Piers Morgan atoa wito wa meneja wa Arsenal Arsene Wenger kuachia madaraka na kubadilishwa na kumkabidhi nafasi hiyo Rais Donald Trump. Kwa mujibu wa Mwandishi huyo anataka Wenger ambaye hajashinda taji la ligi la Uingereza kwa takribani miaka 14 sasa na kubadilishwa na nafasi hiyo apewe Trump kwa sababu anaweza kujenga ukuta mzuri wa mabeki.

Piers amethibitisha mahojiano yake ya kipekee na Rais wa Marekani kwenye kurasa zake za Twitter na pia alituma picha akionyesha jezi ya Arsenal na jina ‘Trump’ liliopo mgongoni wakati ameketi kando ya raisi huyo.

Piers alisema kwamba ‘The moment I invite President Trump to be Arsenal’s new manager – because he’d build a strong defensive wall, have an attacking philosophy and want to win big trophies at all costs.’

Kwa sasa Arsenal wanashika nafasi ya sita na wako pointi tatu nyuma ya klabu ya Tottenham na pointi 5 nyuma ya klabu ya Liverpool ambao wanashika nafasi ya ya nne, ambao ndio nafasi ya mwisho ya kushiriki Ligi ya Mabingwa.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents