Habari

Trump ashtushwa na majaribio ya nyuklia ‘Korea Kaskazini ni hatari kwa Marekani’

Rais wa Marekani, Donald Trump ameshtushwa hatua zinazofanywa na Korea Kaskazini za majaribio ya silaha za Nyuklia ambazo Umoja wa mataifa uliionya kuacha kuzalisha silaha hizo huku akisema kitendo hicho kinahatarisha usalama wa nchi yake.

Rais wa Marekani, Donald Trump

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais Trump amesema kauli zinazotolewa na nchi hiyo na vitendo vya majaribio ya silaha za nyuklia ni hatari zaidi kwa Marekani.

Matamshi ya nchi hiyo (Korea Kaskazini) na vitendo vyake vinandelea kuwa vyenye hatari kubwa zaidi kwa Marekani,” ameandika Rais Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter.

SOMA ZAIDI – Jaribio la siri la nyuklia nchini Korea Kaskazini laleta tetemeko la ardhi

Mapema leo Korea Kaskazini imethibitisha kufanya jaribio la silaha za nyuklia usiku wa kuakia leo kitendo ambacho kimesababisha tetemeko la ardhi baadhi ya maeneo nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents