Habari

Trump atangaza hali ya dharura kuilinda mifumo ya kompyuta dhidi ya maadui wa Marekani, wachambuzi wadai ailenga kampuni ya Kichina ya Huawei

Rais Donald Trump ametangaza hali ya dharura kwa ajili ya kuilinda mifumo ya kompyuta dhidi ya ” wapinzani wa kigeni”

Wachambuzi wanasema uamuzi wa Bwana Trump unailenga kampuni kubwa ya mawasiliano ya Kichina Huawei.

Rais huyo wa Marekani amesaini sheria ya utaratibu wa utendaji ambayo inazuwia mara moja makampuni ya Marekani kutumia mawasiliano ya kigeni yanayoaminiwa kuhatarisha usalama wa nchi hiyo.

Bwana Trump hataji kampuni yoyote katika agizo hilo.

Muasisi wa Huawei Ren Zhengfei aliwahi kusema kuwa Marekani haiwezi kumaliza biashara zake

Muasisi wa Huawei Ren Zhengfei aliwahi kusema kuwa Marekani haiwezi kumaliza biashara zake

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Hata hivyo, wachambuzi wanasema uamuzi huo unailenga kampuni kubwa ya mawasiliano ya Kichina Huawei.

Nchi kadhaa- Marekani ikiwemo- zimekwisha elezea wasi wasi wake kwamba huduma za kampuni hiyo zinaweza kutumiwa na Uchina kwa upelelezi. Huawei imesema kuwa kazi yake haisababishi tisho lolote.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya White House, agizo la Bwana Trump linalenga “kuilinda Marekani dhidi ya wapinzani wake ambao wamekuwa wakionekana kubuni mbinu za kutumia taarifa na mifumo ya teknolojia ya mawasiliano pamoja na huduma zake “.

Huawei ndio kampuni kubwa zaidi duniani inayotengeneza vifaa vya mawasiliano

Sheria hiyo ya rais inampatia mamlaka waziri wa biashara nchini humo ya “kuzuwia shughuli zinazo hatarisha hatari isiyokubalika kwa usalama wa taifa “, iliongeza taarifa.

Hatua hiyo iliafikiwa mara moja na mwenyekiti wa Tume ya kitaifa ya mawasiliano Ajit Pai, ambaye amesema katika taarifa yake kwamba ilikuwa ni “hatua muhimu kuelekea kuilinda mitandao ya Marekani “.

Huawei imekwishakana kuwa inasababisha hatari yoyote katika mawasiliano ya nchi yoyote ile

 

Marekani tayari ilikuwa imewekea masharti mashirika ya mawasiliano nchini humo ya kutumia huduam za Huawei na imewataka washirika wake kuacha kuitumia, huku Australia na New Zealand zote zikiwa zimezuwia matumizi ya Huawei katika mifumo ijayo ya mawasiliano ya simu za mkononi ya 5G. Lakini Huawei inakana kabisa shutuma hizo.

Wakati huo huo , mwenyekiti wake Liang Hua alisema ” iko tayari kusaini makubaliano ya kutofanya ujasusi na serikali” wakati wa mkutano mjini London Jumanne, kutokana na hofu ikiendelea kuongezeka juu ya usalama wa huduma zake zinazotumia mitandao ya simu za mkononi 5G .

Hatua ya hivi karibuni ya Bwana inatarajiwa kuchochea uhasama katika mahusiano yake na Uchina, ambayo tayari yamekwishaingia doa kufuatia vita vya kibiashara vinavyoendelea baina ya nchi mbili.

Marekani iliongeza mara dufu ushuru kwa bidhaa kutoka uchini kwa kiwango cha dola bilioni 200 siku ya Ijumaa na Uchina ikajibu kwa kupandisha juu viwango vya ushuru kwa bidhaa kutoka Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents