Burudani

Trump azuru Palestina na Israel kwa ulinzi mkali

Baada ya kumaliza ziara yake nchini Saudia Arabia ,Rais wa Marekani Dolnad Trump, amewasili nchini Israel na maeneo mengine ya Palestina mapema leo na kuendelea na ziara yake katiaka mataifa hayo.

Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas,na kuingia nao mkataba wa Amani. Israel na Palestina wamekuwa katika mgogoro wa kugombea eneo la WestBank uliopo ukingo wa Magharibi na Mashariki ambao,Israel huuchukulia mji wote wa Jerusalem kuwa mji wake mkuu, nao Wapalestina huchukulia maeneo ya mashariki ya mji huo kuwa makao makuu yake.

Katika mkutano wa siku ya jumapili kwa wakuu wa viongozi wa Kiislamu na Kiarabu mjini Riyadh, Trump aliwataka viongozi hao kuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha wanakabiliana na wanamgambo wa Kiislamu pamoja na wapiganaji wenye itikadi kali.

Huu ni muendelezo wa ziara ya Raisi wa Marekani Dolnad Trump aliombatana na mkewe Melania. Tayari rais huyo ameshatembelea nchi mbili mpaka sasa na amebakiwa na nchi kama Ubelgiji,Vatican na Sicily.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents