Habari

Trump kuitoa Marekani katika mkataba wa Silaha na Urusi

Trump kuitoa Marekani katika mkataba wa Silaha na Urusi

Marekani itajitoa kutoka mkataba wa silaha za nyuklia na Urusi, kwa mujibu wa rais Donald Trump.

Akihutubia waandishi wa habari Trump alisema Urusi ilikiuka mkataba wa mwaka 1987 unaofahamika kama Intermediate-Range Nuclear Forces (INF)

Mkataba huo ulipiga marufuku makombora yanayorushwa kutoka ardhini ambayo yanaweza kusafiri umbali wa kati ya kilomita 500 na 5,500.

“Marekani haiwezi kuiruhusu Urusi kuendelea kuunda silaha huku sisi hatuundi,” Trump alisema.

Mwaka 2014 Rais Obama aliilaumu Urusi kwa kuvunja makubaliano ya INF baada ya kulifanyia majaribio kombora moja la masafa ya wastani.

Wasiwasi kuhusu hatua ya Urusi ya kuunda makombora yanayokiuka mkataba wa INF ni kitu kinachoighadhabisha serikali ya Trump. Lakini uamuzi wa Trump wa kujitoa ni pigo kubwa katika suala la kudhibiti silaha.

Mikhail Gorbachev and Ronald Reagan signing the INF treaty in 1987Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKiongozi wa Usovieti Mikhail Gorbachev Rais wa Marekani Ronald Reagan walisaini INF mwaka 1987

Wataalamu wengine wanaamini kuwa mazungumzo yangeendelea kujaribu kuleta Urusi kwenye makubaliano.

Marekani inasisitiza kuwa Urusi ilivunja mkataba huo kwa kuunda kombora jipya la masafa ya wastani kwa jina Novator 9M729 – linalofahamika kwa Nato kama SSC-8.

Linaiwezesha Urusi kufanya shambulizi la nyuklia kwa nchi za Nato kwa onyo fupi sana.

Urusi haijasema chochote kuhusu kombora jipya lakini imekana kuwa ilikiuka makubaliano.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents