Habari

Trump: “Marekani kuwa na wagonjwa wengi wa Corona ni heshima”

Rais Donald Trump amesema ni ” ni heshima ” kuwa Marekani ina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona duniani.  ”Ninalitazama suala hili kama heshima fulani, kama jambo zuri kwasababu inamaanisha kuwa vipimo vyetu viko vizuri,” alieleza akiwa Ikulu ya Marekani.

Marekani ina watu milioni 1.5 walioathiriwa na virusi vya corona na karibu vifo 92,000, kwa mujibu wa takwimu zinazokusanywa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Nchi inayoshika nafasi ya pili ni Urusi ikiwa na maambukizi ya watu 300,000.

Trump amesema nini?

Siku ya Jumatatu, Bwana Trumo alikuwa akihodhi mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri tangu kuanza kwa mlipuko wa virusi hivyo nchini Marekani.

Aliwaambia waandishi wa habari, ”unajua unaposema kuwa tunaongoza kuwa na watu wengi walioambukizwa, ni kwa sababu tuna vipimo vingi kuliko mtu mwingine yeyote.”

”Hivyo tuna watu wengi walioambukizwa,” aliendelea, ”Sitazami kama jambo baya, ninalitizama kwa heshima fulani, kama jambo jema kwa sababu ina maanisha kuwa tuna vipimo vizuri.”

Aliongeza: ”Hivyo ninaliona kama nembo ya heshima. Kweli ni heshima.

”Ni heshima kwa vipimo na kazi ambayo wataalamu wameifanya.”

Kwa mujibu wa kituo cha kupambana na kudhibiti magonjwa , Marekani imepima watu milioni 12.6 mpaka siku ya Jumanne.

Trump alikuwa akijibu swali kuhusu kama alikuwa akifikiria kuweka marufuku ya kusafiri kwenda Amerika ya Kusini hasa Brazil. Nchi hiyo ni ya tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya waathirika wa virusi vya corona, ikiifuata Marekani na Urusi.

Kamati ya uongozi ya kitaifa ya chama cha Democratic imekosoa kauli ya Trump, ikisema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa kuwa na waathirika wa Covid-19 milioni 1.5 nchini Marekani kunaonesha ”kushindwa kabisa kwa uongozi”.

Je, Trump yuko sahihi?

Wakati marekani ikiwa imefanya vipimo zaidi kuliko nchi nyingine yoyote, si ya kwanza duniani kwa ulinganifu wa idadi ya watu na vifo nchini humo kwa mujibu wa takwimu za chapisho la kisayansi la Our World in Data la Chuo Kikuu cha Oxford.

Katika chati Marekani ya 16 kwa vipimo kwa watu 1,000 ikiwa mbele ya Korea Kusini, lakini nyuma ya Iceland, New Zealand, Urusi na Canada.

Katika kipindi cha juma lililopita, Marekani imekuwa ikifanya vipimo kwa watu 300,000 na 400,000 kwa siku, kwa mujibu wa mradi uitwao Covid Tracking, zikiwa ni jitihada za watu waliojitolea.

Lakini Mkurugenzi wa taasisi ya afya ya Global Health Ashish Jha juma lililopita aliuambia mkutano wa Congress kuwa: ”Marekani inahitaji vipimo zaidi ya 900,000 kila siku. Kwa sasa tuna theluthi tu ya vipimo.”

Marekani pia imeripoti vifo vingi vinavyotokana na virusi vya corona kuliko nchi nyingine yoyote, ingawa kwa ulinganifu wa idadi ya watu na vifo Marekani ni ya sita nyuma ya Ubelgiji, Uingereza na Ufaransa, kwa mujibu wa takwimu za Chuo cha Johns Hopkins

Viwango vya upimaji wa virusi vya corona vimekuwa vikikosolewa na pande zote mbili.

Katika bunge la seneti juma lililopita, Mitt Romney, kutoka chama cha Republican, alikosoa rekodi za vipimo vya nchi hiyo, akisema kuwa ”hakuna cha kushangilia” kwa sababu , alisema ”tulishindwa kufanya jitihada hizo mwezi Februari na Machi”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents