Tupo Nawe

Trump: Nakunywa dawa za Malaria kujikinga na Corona 

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema jana kuwa amekuwa akinywa dawa ya malaria aina ya hydroxychloroquine, kwa muda wa wiki moja na nusu sasa, ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ikulu ya White House, Trump alisema amesikia simulizi nyingi nzuri kuhusu dawa hiyo. ”Na unaweza kushangaa watu wangapi wameitumia na hasa wafanyakazi walioko mstari wa mbele kabla ya kuambukizwa.

Wafanyakazi walioko mstari wa mbele – wengi wanaitumia. Na mimi naitumia, naitumia hydroxychloroquine, sasa hivi, ndiyo”, alisema Trump.

Wataalamu wa Umoja wa Ulaya hata hivyo, wanasema hawaoni ushahidi wowote kwamba dawa hiyo inafanya kazi dhidi ya COVID-19, na tafiti kadhaa zinaendelea kufanyika kufafanua suala hilo.

Dawa hiyo inadaiwa kuwa na madhara na inaweza kusababisha matatizo makubwa ya moyo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW