Habari

Tsh milioni 240 kumrudisha Okwi Msimbazi

Klabu ya Simba imekubali kulipa dola za Marekani 120,000 (mabazo ni zaidi ya Sh milioni 240 kwa klabu ya Sonderjiske ya Denmark ili kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani, Mganda Emmanuel Okwi.
okwi-kaburu

Baada ya klabu hiyo kukamilisha kulipa kiasi hicho cha fedha, mchezaji huyo atarejea kuichezea Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Simba ilimuuza Okwi kwa dola 100,000 mwaka juzi Denmark, lakini kutokana na mchezaji huyo kutopata nafasi ya kucheza Ulaya, imeamua kumrejesha na makubaliano yamefikiwa Sh milioni 240.

“Dola 120,000 tu wale jamaa wanataka watuachie Okwi. Na Okwi naye atasaini kwa mshahara tu mkataba wa mwaka huu, hatumpi dau la kusaini yeye,”kimesema chanzo kutoka Simba.

Taarifa za mitandao ya kujamii jana zilieleza kuwa, Okwi ni mchezaji aliyeipa faida kubwa Simba ndani na nje ya uwanja wakati ule akiichezea klabu hiyo ya Msimbazi.

Mbali na kuwasaidia Wekundu hao wa Msimbazi kushinda matajii mbalimbali tangu ajiunge nao kwa mara ya kwanza mwaka 2010, mchezaji huyo pia aliinufaisha kifedha Simba.

Simba ilimuuza Okwi Etoile du Sahel ya Tunisia Januari mwaka 2013 kwa dau la rekodi kwa klabu za Tanzania, dola 300,000, ingawa baada ya muda akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo ya Tunisia. Mtafaruku ulianza baada ya Okwi kuchelewa kurejea mjini Sousse mkoani Sahel baada ya ruhusa ya kwenda kuichezea timu yake ya taifa, Uganda.

Okwi naye akadai Etoile walikuwa hawamlipi mishahara na kufungua kesi FIFA, ambayo mwisho wa siku alishinda kwa kuruhusiwa kutafuta timu nyingine ya kuchezea kulinda kipaji chake, wakati wa mgogoro wake na klabu ya Tunisia.

Okwi akajiunga na SC Villa ya kwao, Kampala katikati ya mwaka 2013 na Desemba mwaka huo, akahamia Yanga. Hata hivyo, Okwi akavunja Mkataba na Yanga Agosti mwaka 2014, baada ya timu hiyo ya Jangwani kushindwa kumlipa dola za Marekani 60,000 kama ilivyokuwa katika mkataba baina yao na kurejea klabu yake ya zamani, Simba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents