Technology

TTCL kuondoa wazee na kuajiri vijana watakaoiwezesha kuhimili ushindani

Siku za waajiriwa wazee kwenye kampuni ya simu Tanzania, TTCL zinahesabika. Ni kwasababu sekta ya mawasiliano kwa sasa imekuwa na ushindani mkubwa hivyo inahitaji vijana wabunifu na wanaoenda na wakati.

13298259_261567224232792_2022338966_n
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mh. Prof Makame Mbarawa akimpongeza Afisa Mkuu Mtendaji wa TTCL Kamugisha Kazaura baada ya kuzindua nembo mpya hivi karibuni

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema wakati umefika kwa wazee wanaofanya kazi TTCL, kuwaachia vijana.

Alisema hayo wakati akizindua nembo mpya ya kampuni hiyo na mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE wiki iliyopita. Profesa Mbarawa alisema wazee wamekuwa watu wa kuzungumza zaidi ofisini, kuliko kufanya kazi na kubuni mbinu mpya zenye kuhimili ushindani.

13249629_1021836424576348_1770398696_n

Alisema uzinduzi wa nembo mpya katika kampuni hiyo, hautakuwa na maana ikiwa wafanyakazi wa kampuni hiyo hawatabadilika na kutoa huduma zitakazowavutia wateja. Aliishauri menejimenti kutoajiri watumishi kwa kujuana, bali watoe fursa kwa vijana wenye uwezo wa kuhimili ushindani unaotokana na mabadiliko ya teknolojia ya mawasiliano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents