Burudani

Tubanane ya Adasa kutoka Kenya yaongoza orodha kusikilizwa zaidi kupitia platform za muziki Kenya

Tubanane ni kibao kipya kutoka kwa msanii Adasa wa nchini Kenya, na kimeingia kwenye historia kwa kusikilizwa, kupakuliwa na kusambazwa na mashabiki wa muziki kwenye mtandao wa BoomPlay. Kibao Waah chake Diamond na mkongwe kutoka Congo DRC Koffi Olomide kiko katika nafasi ya pili huku kibao kipya chake msanii Fena Gitu kwajina Ngoma kikichukua nafasi ya Tatu.

Adasa ambaye yupo chini ya lebo inayokua kwa kasi Africa Mashariki ya Dallaz Empire amekua kipao mbele kupendwa na wafuasi wa muziki Africa Mashariki huku akiwa na mda mchache tokea aingie kwenye ulingo wa muziki rasmi. Sauti yake nyororo, uandishi na madoido yake yanampa fursa yakukubalika na wengi kwenye muziki.

Imeandikwa na @changez_ndzai – Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents