Tuesday Kihangala kuja na tamthilia ya High Heels mwakani

rayuu

Muongozaji na muigizaji wa filamu nchini Tuesday Kihangala aka Mr Chuzi anatarajia kuja na tamthilia mpya ya TV iliyopewa jina ‘High Heels’.

Tamthilia hiyo itakuwa na waigizaji wengi wa Jumba la Dhahabu ambao ni pamoja na Jini Kabula,Rayuu, Kojack,Bi Moza, Kilomani,Badi,Kishoka na wote waliokuwepo kwenye Jumba la Dhahabu.Pia kutakuwepo na wasanii wengi wachanga.

Akiongea na Bongo5, Rayuu ambaye ataigiza kwenye tamthilia hiyo amesema High Heels itakuwa zaidi ya Jumba la Dhahabu.

“Wajipange wauza sura, ni funiko babkubwa kwani kila mtu kapania kuonyesha uwezo wake,” amesema Rayuu.

Rayuu
Rayuu

“Humo utakutana na utapeli uchawi ujambazi mapenzi visasi nk. Sasa hifh katiki hii ndani ndo utaelewa kwanini imeitwa viatu virefu na pia kwa Tanzania itaanza kutoka kwenye DVD ndo itarushwa kwenye TV.”

Rayuu amesema tamthilia hiyo itaanza kuonekana nchini mwezi January mwakani pamoja na nje ya nchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents