BurudaniDiamond Platnumz

Tufute taswira kuwa muziki ni ubinafsi – Diamond

Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema watu waondoe dhana kuwa muziki ni ubinafsi ili wasanii wa Tanzania waendelee kufanya vizuri katika tuzo za kimataifa.

Akizungumza katika mapokezi ya Rayvanny aliyewasili nchini hapo jana kutoka Marekani baada ya kushinda tuzo ya BET 2017 katika kipengele cha International Viewers Choice, Diamond amesema ndio sababu ya yeye kuanzisha label ya WCB ili kusaidia wasanii na sio kufanya biashara.

“Tufute taswira kuwa muziki ni ubinafsi ili tuhakikishe kila mwaka tunaleta tuzo nyumbani, image isingekuwepo WCB record label huu mwaka mimi sijaingia BET ina maana tusingeleta ushindi nyumbani lakini imekuja kwa namna nyingine. Lengo la kuanzisha WCB record label kuna vijana wengi mtaani wenye talent lakini hawajapata nafasi lakini tunashukuru kila mtu tukimuona na kumleta anafiki mbali,” amesema Diamond na kuongeza.

“Kwanza kabisa kwenye record label usiwe na fikra ya ufanya biashara, ujione kama mtu mwenye passion na hiki kitu unataka kukifanya kifanikiwe. Kwa hiyo tunajitahidi kutengeneza msingi mzuri wa kutengeneza sent mbili tatu zitazoweza kufanya zile kazi mara kwa mara, Mungu katujalia tuna studio lakini je video, kwa hiyo tunajaribu kuweka system na ushirikiano na watu tofauti tofauti,” ameeleza Diamond.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents