Michezo

Tuhuma za ubakaji zamuondoa Cristiano Ronaldo timu ya taifa

Tuhuma za ubakaji zamuondoa Cristiano Ronaldo timu ya taifa

Kufuatia tuhuma zinazomkabili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno pia klabu ya Juventus kutoka Italia Cristiano Ronaldo ameamua kujitoa kwenye kikosi cha timu ya taifa katika mechi mbili zinazofuata ambazo ni kati ya Poland pamoja na Scotland.

Ronaldo anatuhumia kumbaka mwanadada mmoja nchini Marekani anayejulikana kwa jina la Kathryn Mayorga mwenye umri wa miaka 34 ambapo inadaiwa tukio hili lilitokea mwaka 2009 nchini Marekani na Ronaldo inasmekana alimlipa millioni 794, Ingawa mchezahi huyo alizikanusha taarifa hizo

Ronaldo ataukosa mchezo wao dhidi ya Poland katika michuano ya UEFA Nation League ambao utafanyika mwezi Octoba tarehe 11 huku siku tatu baadaye wakicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Scotland.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents