Habari

Tuhuma za watuhumiwa wa dawa za kulevya kuishi kifahari gerezani latinga bungeni

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema hakuna ukweli wowote kuwa baadhi ya watuhumiwa ambao walihusika na dawa za kulevya wanapokuwa gerezani wanaishi maisha ya kifahari.

Hayo yameelezwa leo bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Faharia Hamisi aliyehoji;

Kwakuwa baadhi ya vyombo vya habari vilizungumzia kwamba baadhi ya watuhumiwa ambao walihusika na dawa za kulevya wanapokuwa gerezani wanaishi maisha ya kifahari Je, tuhuma hizi zina ukweli?

“Kuhusiana na ukweli wa tuhuma zinazosambazwa kimsingi si za kweli, nimhakikishie Muheshimiwa mbunge na wananchi kwa ujumla kuwa Jeshi la Magereza linafanya kazi zake kwa kuwasimamia na kuwahifadhi wafungwa ikiwa ni kiuwarekebisha tabia kwa umahili na uamakini wa hali ya juu,” amesema Masauni.

“Sio rahisi na sisi katika kufuatilia kwetu ambapo tumekuwa tukifanya ziara hizi mara kwa mara tumeshuhudia jinsi ambazo askari wa jeshi la Magereza zinafanya kazi yake vizuri na kwa weledi wa hali ya juu kwahiyo tuhuma hizo kimsingi sio za kweli naomba Watanzania wazipuuze.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents