Burudani ya Michezo Live

Tukio la Adam Salamba wa Simba kuomba kiatu kwa Ever Banega wa Sevilla lawa gumzo (Video)

Ukiachana na tukio la klabu ya Simba kufungwa na Sevilla 5-4, lakini bado kuna matukio mengine yanaendelea kuzunguka kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vyombo mbalimbali vya habari.

Kwa sasa tukio ambalo linazungumzwa zaidi ni tukio la mchezaji wa Simba, Adam Salamba kuomba viatu kwa mchezaji mahiri wa Sevilla, Ever Banega. Wadau wengi wanadai tukio hilo lilikuwa sio tukio la kawaida kwani linawashushia heshima wachezaji wa Simba.

 

 

Tukio la Adam Salamba kwenda kuomba viatu vya staa wa Sevilla FC Ever Banega ni tukio la kawaida kuomba kitu cha kumbukumbu kutoka kwa mchezaji mwenye CV kubwa kama Banega anayecheza kikosi kimoja cha timu ya Taifa na Lionel Messi.
.
Tukio kama hilo liliwahi kutokea December 18 2013 Morocco katika mchezo wa FIFA Club World Cup kati ya Atletico Mineiro ya Brazil na Raja Casablanca ya Morocco iliyomaliza game hiyo kwa ushindi wa 3-1, wachezaji wa Raj baada ya hapo walikuwa wanawania kupata jezi ya Ronaldinho na wengine kugawana kiatu kimoja kimoja kama ukumbusho

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW