Tragedy

Tukio la tindikali Zanzibar lawachefua Watanzania na raia wengine, soma maoni mbalimbali hapa

“Disgusting, sick men. I won’t be going to Zanzibar any time soon thanks, ni maoni ya Shirley Bisschoff aliyoyatoa kwenye mtandao wa New24 wa Afrika Kusini huku – Mike North wa Uingereza akiandika kwenye mtandao wa Daily Mail wa Uingereza, “Another reason never to go to these pitiful countries leave them well alone , crazy.”

article-2387651-1B381DE8000005DC-830_634x783
Katie Gee, aliyefunikwa blanketi akiwa na mama yake wakiingia hospitali baada ya kusafirishwa kutoka Zanzibar

Maneno hayo yanatosha kuonesha picha halisi ya namna tukio la kumwagiwa tindikali wasichana warembo, wenye umri msogo, wasio na hatia na walioamua kuacha raha za kwao Uingereza kwenda kujitolea kufundisha watoto yatima visiwani Zanzibar, linavyoweza kuathiri sekta ya utalii katika visiwa hivyo.

“Tourism is the second-biggest foreign-exchange earner in Tanzania after mining and any lasting damage to the country’s reputation abroad could hurt industry revenues,” wameandika New24.

Katie Gee na Kirstie Trup ambao wote wana umri wa miaka 18 kwa sasa wamelazwa kwenye hospitali ya Chelsea and Westminster nchini Uingereza kutibiwa majeraha yao yaliyotokana na kumwagiwa tindikali hiyo.

Mungu ndio anajua ni idadi ya watalii wangapi walioghairi kwenda Zanzibar kupumzika kuhofia usalama wao baada ya tukio hilo.

Haya ni baadhi ya maoni ya Watanzania na raia wengine waliyoyatoa kwenye kurasa Za Facebook NA Twitter za Bongo5 kuhusiana na tukio hilo.

Jeannette L. Ladyj

Few of you can’t destroy the pride of the whole country! Jifunzeni utu na kuwaza kabla ya kutenda. Upumbavu huu!!! Nnavyoisifia Nchi yetu! Loo!?

Olivia Mosses

Inasikitisha na kufedhehesha,tabia mbaya sana maisha yatakapo kua magumu kwa kukosa watali ndo mtashika adabu na kulima hawajui….aibu tupu mwaka huu.

Macharia Gladys

Very very sad I thought Zanzibar as a peaceful place full of beauty am scared will never go there its painful the thought of those 2 gals. So why can’t I sing or be myself and enjoy life ? Nobody gets offended in Christianity just coz somebody has sang a song or wore their small or long clothes? this is just crazy and inhuman c’mon Zanzibar you’ve hit below the belt.

Sebastian Godfrey

Watu watumie akili na utu wawaze kabla ya kutenda sasa zenji mnaingia hasara kwenye utalii, dunia sasa hivi ni kama mtaa habari zimefika kwingi unadhani watakua na amani ya kuja huko mmekosa kazi inabid mpelekwe kwenye mapori mkalime mmeniboa baadhi ya wafwata mkumbo na ukikamatwa utafungwa hadi libomoke ndo utoke.

Lister Osward

Hii nchi ya Tanzania siku hizi inapata sifa mbaya sana. Sijui tunakoelekea ni wapi kwa kweli..MUNGU TUSAIDIE

Lord Herry

It’s serious matter for our country we should do some thing other wise our tourism sector will be doom,I fill So sad for the girls. I wish they get caught. It’s sad and painful for me also for there family,I wish them get well and speed recovery.

Hika Lyimo

This act brought shame to our country…its sad, how big of an impact this will cause on so many levels.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents