Burudani

TUMA yahitaji wanachama zaidi

Mkoloni

Mwanamuziki na mwenyekiti wa muda wa chama cha TUMA (Tanzania Urban Music Association) Fred Maliki ‘Mkoloni’ ametoa taarifa kwa wasanii wasamabazaji na madj wote kwamba umefika kipindi cha kujiunga na kuwa kitu pamoja.

Akizungmza na Bongo5, alisema wanawaruhusu Madj, ambao wanahusika na kupiga muziki katika mastudio na sehemu mbalimbali, wasambazaji wadogowadogo ‘Wamachinga’, Wasanii Waandishi  na hata mtu yoyote ambaye anahitaji kupata kazi za wasanii au taarifa za wanamuziki wanachama. Alisema hadi sasa wameshafikikia zaidi ya wanachama 170, wakiwa wasambazaji Madj na wasanii, ila kujiunga bule na kupewa uawachana wa kudumu.

Aidha alibainisha wanachama wa kudumu wa TUMA, watapa faida mbaalimbali, kwa kujiunga na  kupata Huduma za Hospiali tano hapa nchini bule, kama ilivyokuwa kwa vyama vingine.  Alisisitiza kwa kusema chama hicho si kigeni kwani makazi yake yapo Dae es salaam na kilianzishwa mwaka 2004, kikiwa kimesajiriwa chini ya balaza la sanaa Tanzania ‘BASATA’.

Alisema kipindi hicho Mwenyekiti akiwa K.Bazil, katibu Stara thomas na katibu mwenezi ni Joseph Mbilinyi ‘Sugu’. Hata hivyo alisema baada ya hapo watu wenye tamaa wakaanzisha vyama vingine, ambavyo havikusajiriwa lakini wakawa wanawalaghai wasanii, na kuwafanya wawe maskini.

Alidai kwamba wao hawakuchoma kupitia BASATA, wakaomba msaada kwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Ndg Jakaya Mrisho Kikwete  walipiwe fedha  za jenga. Alisema hata hivyo walisikia zimetolewa shilingi milioni 225, walizoomba wao kwa kila mwaka, lakini chaajabu hazikufika mikononi mwao.

Alimalizia kwa kusema watu waache kuanzisha vyama kwani TUMA, ipo kwaajiri ya wasanii wote wa BongoFleva,na kila mtu anayetaka kugombea cheo chochote ajiunge na agombee kuliko kuanzisha chama kingine na kuwagawanya waasanii.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents