Tia Kitu. Pata Vituuz!

Tume ya uchaguzi DRC yaeleza sababu Za matokeo ya uchaguzi kucheleweshwa

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu huenda yakachelewa na kupita tarehe iliyotarajiwa ya Januari 6.

Kwa mujibu wa BBC, Rais wa tume hiyo, Corneille Nangaa, amesema kituo kikuu cha kuhesabia kura bado kinasubiri matokeo ya zaidi ya asilimia 80 ya kura zilizopigwa kutoka vituo mbalimbali kote nchini humo.

Aidha amesema bado ni mapema mno kubaini chanzo cha kuchelewa kwa matokeo hayo, lakini vyama vya upinzani vinadai hiyo ni njama ya kuiba kura.

Wakati huo huo shirika la Umoja wa Afrika pamoja na Shirika la Kimaendeleo la Kusini mwa Afrika – SADC yametaja uchaguzi huo kama ulioendeshwa vizuri kwa kiwango kikubwa, licha ya kuwa na matatizo kadhaa ya kiufundi pamoja na machafuko katika baadhi ya maeneo.

Waangalizi pia wamesema baadhi ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kuchelewa na kusababisha kucheleweshwa kwa zoezi hilo.

Wameongezea kuwa wapiga kura hawakuelimishwa vizuri kuhusu utumizi wa vifaa vya kielektroniki vya kupigia kura ambavyo vimetumika kwa mara ya kwanza nchini humo.

Wakizungumzia changamoto za kuandaa uchaguzi katika maeneo yaliokuwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola na mapigano, Umoja wa Afrika ulishtumu hatua ya kuwafungia baadhi ya wapigaji kura kukamilisha haki yao ya kidemokrasia, huku wakisisitiza kwamba washikadau wa masuala ya kisiasa hawakushirikishwa katika uamuzi huo.

SADC pia wamekiri kwamba huu ndio uchaguzi wa kwanza wa kujitegemea kifedha nchini humo, ikiwa ni hatua muhimu kwa ukuaji wa kidemokrasia.


Wagombea wa upinzani Martin Fayulu (Kushoto) na Felix Tshisekedi (Kulia) wanashindana na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Shadary (Kati)

Shirika la Umoja wa Afrika linatumaini kuwa matokeo yataakisi uamuzi wa wananchi, na kuwataka wale ambao hawatokubaliana na matokeao hayo kufuata njia ya haki ya sheria kuupinga.

Wagombea wakuu wa urais DR Congo

MARTIN FAYULU (MUUNGANO WA LAMUKA) Muungano wa Lamuka

EMMANUEL RAMAZANI SHADARY Common Front for Congo (FCC)

FELIX TSHILOMBO TSHISEKEDIUnion for Democracy and Social Progress (UDPS)

“Lazima tkubali kwamba nchi hii ni kubwa mno, kwa hivyo kukusanya matokeo na taarifa zozote zile sio kazi rahisi. Kwa hivyo itatubidi tusubiri tuone itachukua muda gani kuchukua hesabu zote,” amesema Joseph Malanji ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa zambia na ambae alikuwa kiongozi wa waangalizi wa shirika la SADC.


Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 17

Nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati ina utajiri wa madini na ndiyo mzalishaji mkubwa wa madini ya cobalt, yanayotumiwa kwa simu na betri za magari.

Lakini ina viwango vya juu vya umaskini, miundo msingi duni na wanasiasa na wafanyabiashara wanalaumiwa kwa kujitajirisha huku wengine wengi wakibaki kuwa maskini.

Imekuwa kwenye hali ambayo waangalizi wengine wanataja kuwa vita vya dunia vya Afrika kati ya mwaka 1997 na 2003.

Mawasiliano ya interneti yamekatizwa kwa siku ya nne sasa, na kulingana na serikali hatua hii ni kujaribu kuzuia watu kusambaza matokeo ya udanganyifu ya uchaguzi.

Hali hio inatazamiwa kuendelea hadi pale matokeo yatakapo tangazwa, hatua ambayo haijaufurahisha upinzani.

Presentational grey line

Nani waliwania?

Kulikuwa na wagombea 21 lakini watatu ndio wakuu:

  • Emmanuel Ramazani Shadary, Waziri wa zamani wa mambo ya ndani na mtiifu kwa Kabila, ambaye aliwekewa vikwazo na Muungano wa Ulaya kwa hatua zilizochuliwa upinzani wakati wa maandamano ya mwaka 2017.
  • Martin Fayulu, Mkurugenzi mkuu wa zamani wa mafuta ambaye ameahidi nchi yenye mafanikio lakini ambaye watu maskini wanahisi hawezi kuwatetea.
  • Felix Tshisekedi Tshilombo, Mtoto wa mwanasiasa mkongwe ambaye ameahidi kupambana na umaskini.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW