Habari

Tume ya Uchaguzi mkuu nchini Gabon yamtangaza Ali Bongo mshindi wa urais

Wanachama wa tume ya Uchaguzi mkuu nchini Gabon wametangaza kuwa rais Ali Bongo, ametetea kiti chake cha urais baada ya kumshinda mpinzani wake Jean Ping.

_90983420_alibongo_gabon_512x288_getty_nocredit

Ushindi huo ni baada ya kumalizika kwa shughuli za upigaji kura, hapo siku ya Jumamosi.

Lakini mwandishi wa habari wa BBC mjini Libreville, amesema kuwa wajumbe wanaowakilisha upinzani katika tume ya uchaguzi, wameondoka ndani ya ukumbi wa kuhesabu na kusawazisha matokeo ya kura, na kukataa kutia saini hati zinazompa ushindi rais Bongo.
Walinda usalama wanapiga doria katika barabara za mji mkuu Libreville huku taharuki ikitanda kote nchini humo.

Familia ya Bongo imetawala Gabon kwa nusu karne huku Omar Bongo akitawala kwa miongo minne, na mwanawe rais wa sasa Ali, alichukua hatamu za uongozi mnamo mwaka wa 2009.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents