Michezo

Tumeghaili hatuendi nje, tutaweka kambi mikoani – Yanga

Uongozi wa klabu ya Yanga umesitisha mpango wa kuipeleka timu hiyo nchini Zambia kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa ngao ya hisani  dhidi ya Simba na maandalizi ya msimu mpya ujao na badala yake wataweka kambi mikoani.

Kikosi cha Yanga kikijifua na mazoezi ya Gym kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Uongozi wa Yanga umesema badala ya kwenda Zambia sasa wanafikiria kuweka kambi kwenye mikoa kati ya Morogoro au Arusha ili kujifua kwa ajili ya maandalizi ya usimu ujao.

Timu itaingia kambini jumanne ijayo lakini sio nje ya nchi, mapendekezo yapo kati ya mikoa ya Arusha na Morogoro, mpaka kufika kesho au kesho kutwa tutajua tutaenda wapi,“amesema Kiongozi mmoja wa Yanga ambaye hakutaka jina lake liandikwe.

Kwa upande mwingine Kiongozi huyo amesema klabu ya Yanga bado ipo kwenye mchakato wa kumtafuta beki mbadala wa Vicent Bossou aliyetemana na klabu hiyo.

Sio kwa Bossou tuu pia Kocha Lwandamina bado hajaridhishwa na kiungo Justin Zulu na amepanga pia kumtafutia mbadala wake“,amesema Kiongozi huyo.

Wakati klabu ya Yanga ikijipanga kuweka kambi mikoani watani wao wa jadi Simba SC wana wiki moja sasa nchini Afrika Kusini walikoweka kambi wakijifua na mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa 2017/18.

Yanga na Simba zitavaana Agosti 23 mwaka huu kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa uwanja wa Taifa, jijini Dare se salaam kabla ya kufungua pazia la Ligi kuu Soka Tanzania bara dhidi ya Lipuli FC.

By Godfrey Mgallah

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents