Michezo

Tumejiandaa kuchukua ubingwa wa VPL 2017/18 – Singida United

Kocha msaidizi wa klabu ya Singida United, Jumanne Chale amesema timu yake inaendelea kufanya maandalizi ya kutosha kwaajili ya kuchukua ubingwa na VPL msimu wa mwaka 2017/18.

Nahodha wa Singida United, Nizar Khalfan

Timu hiyo ambayo inadhaminiwa na SportPesa, imeweka kambi mkoani Mwanza kwaajili ya maandalizi zaidi ya msimu ujao.

Kocha huyo msaidizi amesema tangu wameanza maandalizi ya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya msimu ujao kila kitu kinaenda vizuri huku akidai wachezaji wote wapo vizuri na hakuna majeruhi.

“Kila timu huwa inajiandaa kwa ajili ya kuchukua kombe na sisi kama SIngida tumejipanga kuchukua kombe maana kama unavyoona mazoezi yetu tunafanya kwa siku mara mbili, tunafanya mazoezi kwa nguvu na wachezaji unawaona wapo vizuri na ni wiki ya pili sasa,” alisema Chale.

Aliongeza,”Tutahakikisha tunachukua ubingwa ili tuweze kuleta mageuzi ya soka katika nchi hii kwani tumakamilika kila idara,”

Kwa upande wa nahodha wa timu hiyo, Nizar Khalfan amesema mpaka sasa wanaona wanaendelea vizuri na maandalizi ya msimu ujao.

“Mazoezi ni mazuri tangu tumeanza na mpaka sasa tumeshapata mechi moja ambapo tumeangalia mwenendo wetu wa timu vipi na kwakweli tunaendelea vizuri sana kwani tumanza mazoezi mapema na wachezaji wamezoeana mapema,” alisema Nizar.

Aliongeza, “Timu yetu imebadilika sana tangu tucheze mashindano ya SportPesa Super Cup kwani kipindi kile wachezaji mazoea kulikuwa hamna tofauti na sasa hivi tunacheza vizuri, tunatoa pasi na kila mtu anajua akipiga wapi pasi mwenzake anaweza kuukuta mpira na hicho ndicho kitu kikubwa katika timu.

Aliongeza,”Tuna malengo makubwa kwa msimu ujao na tunataka kuleta upinzani mkubwa na ikiwezekana tuweze kumaliza katika nafasi tatu za juu kwasababu tumefanya usajili mzuri ambao upo makini na mwalimu ana uzoefu mkubwa katika ligi hii ya Vodacom kwani amekuwepo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa kwahiyo anazijua timu zote za ligi. Tuna mwalimu mzuri, tuna kikosi kizuri na tunafanya mazoezi vizuri tupo fiti na uzuri ni kuwa tumeanza mazoezi mapema sana ili wachezaji waweze kuzoeana,”

Timu hiyo ambayo imepanda ligi kuu msimu huu imekuwa na malengo makubwa ya kufanya vizuri ndani ya msimu wake wa kwanza.

Source: SportPesa News

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents